Wednesday, March 25, 2020

FAIDA ZA TOHARA AU KUTAHIRIWA KIAFYA

✂️FAIDA ZA TOHARA KWA WANAUME


👉Tohara
ni upasuaji mdogo wa kukata na kuondoa govi, yaani ngozi inayofunika ncha ya uume.

FAIDA TOHARA KIAFYA

🔴1. USAFI, Kikawaida Ngozi ya uume( govi) huficha uchafu na pia kuzalisha mafuta meupe meupe yanayojulikana kitaalamu kama smegma ambayo huweka mazingira ya wadududu (bacteria kuzaliana) hivyo kusababisha maginjwa

🔴2.KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI

Mtu anapotahili ngozi ya kichwa cha uume huwa ngumu na kuzuia kupata michubuko kiurahisi tofauti na ya mtu ambaye hajatahili hivyo kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kiasi fulani.

🔴3.KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA MAGONJWA ZA ZINAA NA MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO

🔴4.KINGA DHIDI YA SARATANI YA UUME(PENIS CANCER)

utafitiu unaonesha kua saratani ya uume inawapata sana watu ambao hawajatahili

🔴5.KUPUNGUZA HATARI YA KUPATA SARATANI YA SHINGO YA KIZAZI KWA WANAWAKE

Utafiti pia unaonesha kua mwanamke kujamiiana na mtu ambaye hajatahili inamweka kwenye hatari( Risk )ya kupata saratani ya shingo ya kizazi kutokana na uchafu unaotunzwa kwenye govi kuweza kua na Virusi aina ya Human Papilloma Virus (HPV) ambavyo husababisha saratani ya shingo ya kizazi.
✍️🔴 MwanaApp ♥️ online clinic⚕️

No comments:

Post a Comment