HASARA ZA KITAMBI KWENYE TENDO LA NDOA NA NJIA ZA KUJITIBU
✍️Dr.chilo⚕️ online clinic 💞
Kitambi na uzito kupita kiasi ni matokeo ya mafuta mengi mwilini na kutokufanya mazoezi ya viungo.
Mafuta mengi mwilini husababishwa na lishe mbovu ambazo hazizingatii taratibu za afya. Ulaji wa vyakula vyenye mafuta kupita kiasi, na Kula Kula hivyo bila mpangilio ni chanzo cha uzito kupita kiasi na vitambi.
★Hasara za kitambi na uzito kupita kiasi.
1. Uume kuwa mdogo. Kitambi hufanya maumbile ya uume kurudi ndani na kuonekana madogo. Hii ni kutokana na mrundikano wa mafuta kwenye tumbo na maeneo mengine ya mwili ambapo Hali hiyo husababisha uume kuvutwa kurudi ndani na kufanya muonekano wake kuwa mdogo, tofauti na wanaume wembamba huonekana kuwa na maumbile makubwa ya uume.
2. Upungufu wa nguvu za kiume. Upungufu wa nguvu husababishwa na mkusanyiko wa mafuta kwenye mishipa ya damu, ambapo Mafuta hayo huzuia mtiririko wa damu ya kutosha kwenda kwenye Uume, hivyo mtu huyo anashindwa kusimamisha uume wake sawasawa.
3. Shinikizo la damu na magonjwa ya moyo. Hii Pia husababishwa na mkusanyiko wa mafuta kwenye moyo na mishipa ya damu.
⭕★Njia za kupunguza kitambi na uzito kupita kiasi.⭕
⚕️1. Mazoezi ya viungo. Kufanya mazoezi ya viungo husaidia mwili kutengeneza nishati ambayo hufanya kazi ya kuyeyusha mafuta na kujenga afya ya moyo.
⚕️2. Lishe Bora. Epuka ulaji wa vyakula vyenye mafuta mengi na vilivyokaangwa Kwa mfano chips na kitimoto. Pia epuka matumizi ya pombe hususani bia.
⚕️Kunywa maji ya kutosha kila siku angalau Lita 2½.
⚕️Kula Kwa mpangilio asubuhi, mchana na usiku usile kiwango kikubwa Cha wanga.. Sio Kula Kula hovyo bila mpangilio kama ng'ombe.
✍️✍️Toa maoni wewe unakizungumziaje kitambiii .?
No comments:
Post a Comment