Wednesday, April 29, 2020

🍋FAIDA 9 ZA JUICE YA LIMAO ZITAKAZO KUSHANGAZA🍹

🍋🍋UMUHIMU WA KUNYWA JUICE YA LIMAO Au NDIMU KIAFYA.💖💖👇👇


🎯🎯Watalam mbalimbali wa afya wanasema ya kwamba kwa kila siku ni vyema unywe maji ya Limao /ndimu
 ili uweze kujitibu magonjwa na kuimarisha afya yako na Kuwa na muonekano mzuri wa ngozi.

👉👉Unachotakiwa kufanya ni;🎯
✍️✍️Dr.chilo📳 MwanaApp 👩‍⚕️

🍋🍋Weka maji yenye joto kidogo (vuguvugu) katika glasi au kikombe , kata limao au ndimu vipande viwili na kamua kipande kimoja tu ndani ya glasi yenye maji.🍹🍹

🍋🍋Kunywa na uanze siku mpya. Ni vizuri ukafanya hivi dakika 30 kabla ya kula chochote kingine kwa faida zaidi.🍷🥂🍹🍹🍋🍋🍋🍋.


👩‍❤️‍👩👩‍❤️‍👩. Mshirikishe mwenzio ili naye afaidike na elimu hiii 👩‍👩‍👧‍👦👩‍👩‍👧‍👦👩‍👩‍👧‍👦

🎯FAIDA ZA KUNYWA MAJI YA LIMAO .
utajionea Mabadiliko makubwa Kwenye mwili wako.👇👇👇👇🍋🍋

💖1. Huchochea Mmeng’enyo💖

🍋🍋Maji yenye ndimu husaidia chakula kusagika vizuri na haraka katika mfumo wa chakula.
🍋🍋Japo limao lina asidi(acid) lakini likiwa tumboni huwa alkali (alkaline) na kufanya mazingira mazuri kwa usagaji wa chakula.
🍋🍋Pia maji ya uvuguvugu na LIMAO husaidia kupunguza michirizi ya unene sehemu mbalimbali za mwili.

💖2. Huboresha Kinga za Mwili💪

🍋Vitamini C na potasiumu iliyomo kwa wingi katika limao inasaidia katika utengenezaji wa seli za kinga katika mwili Hivyo hukufanya usipate Magonjwa nyemelezi🍋.

💝3. HUSAIDIA KUONDOA FREE RADICALS MWILINI💖


🍋🍋Vitamini C ni antioksidant (antioxidant) ambayo inasaidia kuondoa free radicals mwilini ambazo zimetambulika kusababisha saratani (cancer).
💝4 .Usafishaji wa Mwili na Damu💖

🍋🍋Limao husaidia kusafisha damu kwa kuondoa uchafu. Limao pia husafisha figo ,ini na mfumo wa chakula.

💝5. Dawa ya Kikohozi na Mafua💖

🍋🍋Limao ikitiwa katika maji ya uvuguvugu na asali husaidia sana katika kutibu mafua na kikohozi kwa njia ya asili NA kukufanyia ujisikie vizuri kwa Magonjwa yanayohusu mfumo wa hewa.

 💝6. HUSAIDIA NGOZI ISIZEEKE MAPEMA.💞

🍋🍋Limao inasaidia kufanya ngozi isizeeke. Kama unataka kubaki kijana basi limao litakusaidia. Tabia za vitamin C za kusafisha uchafu zinasababisha kufanya ngozi kuwa na afya na kutozeeka haraka.👇👇

💝💝7. Husaidia Kupungua Uzito💞💞

🎯🎯Limao hupunguza hamu ya kula. Na inajulikana kuwa sababu kubwa ya watu kuwa na uzito mkubwa ni kula chakula kingi au kula mara kwa mara. Limao litakufanya ujisikie kushiba muda mrefu hivyo kusaidia wale amabao wanataka kupungua uzito.

💝💝8. Kuondoa Harufu ya Mdomo🤣🤣
Limao husaidia kuua bakteria wabaya mdomoni ambao husababisha harufu mbaya Ukiwa unaongea hii nikero kubwa .
🍋🍋Ukiwa upo na mpenzi wako akiwa ananuka mdomo ndo utakua ilivyo kero Kama utahitaji tiba na ushauri wasiliana na Dr .chilo uweze kumaliza shida hii
💝💝9.Husaidia Kuondoa harufu mbaya kwapani.
🍋🍋Limao Ni Kitu Muhimu Sana Kwenye Kuondoa harufu mbaya kwapani na Michirizi sehemu mbalimbali za mwili ,ili kuweza Kupata Kanuni za kutumia Limao ili Kuondoa Michirizi na harufu mbaya kwapani
📳📳wasiliana na Dr.chilo kwa WhatsApp number +225755988626.
na install MwanaApp kujifunza mambo mengi ZAIDI ya Afya.👇👇👇👇

 #daktari mkononi#Afya yako mtaji wako🎯🎯💖

Monday, April 27, 2020

🤫Maneno 20 Ambayo Hutakiwi Kumwambia Mtoto Wako🤐


🎯Mara kadhaa wazazi wamekuwa wakiwaambia watoto wao maneno mbalimbali wakati wakiwa na furaha au hasira. Ipo nguvu kubwa kwenye maneno ya kutamkiwa ambayo wazazi wengi hawaifahamu.

💡 Kuna Siri kubwa kwenye kauli unazozitoa juu ya maisha yake ya baadae , hakika maneno yanaweza kujenga au kubomoa maisha ya mtoto kwa kiasi kikubwa.
 🤐 fahamu maneno 20 ambayo hutakiwi kumwambia mtoto wako.🎯

🤐1. Wewe ni mtoto mbaya🤫

Wazazi wengi wanapokasirishwa na mtoto humwambia wewe ni mtoto mbaya, hili humfanya mtoto ajione hafai na itamjengea kutojiamini .

🤐2. Kwanini usiwe kama dada au kaka yako?🤔

🎯Kauli hii humfanya mtoto ajione dhaifu kwa sababu unamlinganisha na wengine. Kauli hii pia humjengea chuki na wivu kwa wale unaowataja kwake kuwa ni bora. Hili husababisha watoto kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na kutopeana ushirikiano Siku wakiwa Wakubwa. pia MTOTO ataona ndani ya familia Kuna ubaguzi.

🤫3. Huwezi hili /unajisumbua tuu🤐

🎯Mwache mtoto ajaribu ashindwe na si wewe kumwambia kuwa hawezi.
"kwani kwenye maisha ni bora ujaribu na ushindwe kuliko kushindwa kujaribu." 💪kama mzazi unapaswa kuwa hamasa kwa mtoto na si kumkatisha tamaa.

🤐🤐4. Usiongee na mimi Tena ukome.

 🤔🤫Kama hautaki mtoto wako aongee na wewe, je unataka aongee na nani? Ukiwa umekwazwa na mambo yako, usihamishie matatizo hayo kwa mtoto.hii itamfanya atengeneze usugu  wa dharau na kibuli kwako mwenyewe.
♥️♥️Kumbuka mtoto naye ana haki ya kusikilizwa, msikilize na umjibu kama inavyotakiwa.

🤐🤐5. KWANINI UNAFANYA VITU KAMA MWANAMKE   ??🤔

🎯👉Kumwambia mtoto neno hili ni kumwonyesha kuwa kuna jinsia fulani bora au yenye nguvu zaidi. Hivyo ni vyema kutokumwambia mtoto neno hili, mwache akue na atatambua mwenyewe kama kuna jinsia dhaifu au yenye nguvu zaidi.

🤐🤐6. Niache/ Usinisumbue🤫🤫

🎯Wazazi wengi hupenda kuwaambia watoto wao “niache” “nina kazi niache” “usinisumbue”, n.k. Kumbuka kuwa wewe ni kila kitu kwa mtoto wako, je unataka akuache aende kwa nani?

🌱🌱Tenga muda na uwe karibu na mtoto wako na kuweza kusikiliza hisia zake.hapo utaweza kugundua kipaji Cha mtoto wako.

🤐7. Hakuna mtu anamtaka mtoto kama wewe ,kwanza sikupendiii🤫

🎯🎯Kuna wazazi huwajengea watoto roho ya kukataliwa tangu wakiwa wadogo sana. Kumwambia mtoto maneno haya humfanya ajione duni na mwenye kukataliwa; hivyo epuka maneno haya ili umkuze mtoto wako VIZURI nae aje akukumbuke ukiwa mzee.

🎯🎯8. Umeshakuwa usifanye Kama MTOTO.👇👇

✍️✍️Kama mtoto anamalizia utoto wake mwache amalizie asije akacheza ukubwani. Mwache afurahie na kuutumia utoto wake vyema kwani kuna kipindi ataacha utoto yeye mwenyewe. usilazimishe kila Kitu akifanye kwa muda unaoutaka wewe.

💪💪9. Wewe ni mvivu/ Ujiwezi /huna unachokijua wewe.

🏋️🏋️Mtoto akishatambua kuwa wewe unamwona ni mvivu, kamwe hawezi kuwa na bidii ya kazi. Mtoto anaposhindwa kufanya kazi vyema, mhamasishe na kumtia moyo badala ya kumwambia wewe ni mvivu / upokama mlenda mlenda tuuu .

😫10. Unaninyima raha wewe mtoto hujui tuuu😏😏

Mara nyingi watoto wanapowakwaza wazazi, wazazi huwaambia kuwa wanawanyima raha. Je kama unamwambia mtoto kuwa yeye siyo chanzo cha furaha kwako ni nani atakayekupa furaha?
😠 itamjengea hofu kila atakapo Kuwa Karibu yako na hawezi kukupaushirikiano wa maono na fikra zake.🙆🙆

🐓11.  lazima ufuate sheria zangu 🤛

🎯 Wazazi Wengi hujifanya mabepali/ na kutangaza utemi kwa WATOTO wao sio zuri kabsa  mpe nafasi Mtoto Kuwa huru kifikra.
🎯utamfanya Mtoto asiwe na uamuzi juu ya maisha yake na Kuwa mtumwa wa fikra zako 👣👣


🎯🎯12. Mali zote hizi Ni zako na nitakufanyia chochote unachotaka.🤸

🧠Inawezekana una mali nyingi ambazo kweli kabisa ni za mtoto wako, lakini unapaswa kumjengea mtoto akili ya kutafuta na si kumpumbaza kwa mali ulizo nazo.🧠🎯

Kumwambia mtoto kila kitu changu ni chako, humfanya asifanye bidii au aone ana haki ya kupata na kutumia kila kitu jinsi apendavyo, utaweza ukaja kujuta baadae kwa Maneno yako .


💖💖13. Nakupenda kuliko watoto wangu wote 💯💯

💘💘 Waswahili wanasema unampa bichwaaaa na kujiona keki .
Kauli hii humfanya mtoto awe mbaguzi na aone kuwa kuna ubaguzi na upendeleo kwenye familia. Hata kama unampenda mtoto fulani zaidi, basi usimwambie mtoto mwingine.
😁😁kauli zako Kuna Siku zitakukosesha Amani🙄🙄

😜14. Siwezi kukukatalia kitu .

🍎🍎 Kauli hii ni mbaya humfanya mtoto akutawale na aone kuwa unatakiwa kutii, kukubali na kumpa kila anachokitaka.kama unaijua kesho yako Basi endelea kumwambia hilo neno🌓


🙋15. Usiongee  au  Usiwatembelee Watu fulani fulani .

HakunaKitu kibaya Kama kurithishwa MAADUI.
Kama una chuki zako, zimalize wewe mwenyewe na si kuzihamishia kwa mtoto. Mtoto anapokuja duniani hutafuta kujenga mahusiano na watu na si kujenga chuki na matengano.

🤲🤲16. Sitakusamehe milele🤝🤝

"Kusamehe mtu aliyekukosea Kuna msaada mkubwa kwa Afya yako ulie samehe kuliko aliyekukosea._"

🙏🙏Mzazi anapaswa kuwa mfano mzuri wa kumfundisha mtoto kusamehe. Ikiwa wewe humsamehi anapokukosea, je unafikiri atakuwa na roho ya kusamehe wengine? Mfundishe mtoto kusamehe.👌👌

🤜17. Ngoja Mtu fulani aje akupige .💔

💗Hii ni kauli inayopendwa sana na wazazi wengi hasa wakina mama ,mama usitengenezee chuki kwa watu wengine 👉 timiza wajibu wako🙋.
Kauli hii humfanya mtoto amwogope baba na amwone kama adui, pia humfanya mtoto amwone mama kuwa ni dhaifu, ikiwa baba hayupo mtoto atafanya makosa kwani anajua mama hamfanyi kitu chochote na hatuwezi.

😥18. Matusi yote  na Majina mabaya.

🎯Mtoto mtukanaji mara nyingi anaishi kwenye familia inayotukana. Utamkuta mama anamwita mtoto mbwa ,mbuzi, ng’ombe, shetani, jambazi, paka, nguruwe,  n.k. je kweli ulizaa vitu hivyo Basi Kama yeye mbwa, Basi wewe utakua mama mbwa Sasa. 🙄Jiulize tuu Siku  akujibu  hata wewe mbwa 👉 Kama unavyoniita👌👌.
Kama nakuona vile itakavyo kuchoma Basi tuache kuita WATOTO Majina mabaya.
📖📙Unapomtukana mtoto, naye hujifunza kuwatukana watu wengine na Siku atakutukana wewe pia mbele za watu. Pia humwathiri kisaikolojia na kiroho na kumfanya awe kama kile unachomwita.

🔪🔪19. Nitakumaliza au nitakuua🔪

Baadi ya wazazi huenda mbali zaidi na kuwaambia watoto wao maneno ya kuwatishia kuwadhuru vibaya au kuwaua.

Hili humwathiri mtoto kisaikolojia na kumjengea tabia ya kuwatishia au kuwadhuru watu wengine. Kama mtoto anatishiwa kuuwawa na wewe ni nani atakayemlinda?
 💡chunga ulimi wako👅


20. Acha kulia haraka au usilie

👁️Kulia ni njia moja wapo ya mtoto kueleza hisia zake. Kumzuia mtoto kulia ni sawa na kumkataza kuweka wazi hisia zake. Mwache alie kama hana maradhi, kwani baada ya muda atachoka na kunyamaza mwenyewe.
Kitendo Cha kulia hata kwa watu wazima HUONGEZA Siku za kuishi.
💡Muombe Mungu akujaria hekima,busara na maarifa ya kumkuza mtoto kwenye tabia unayoipenda *
🎯MUNGU ATIMIZE HITAJI LA MOYO WAKO🙏🙏
✍️✍️DR.CHILO.💡 Asante kwa kusoma hadi Mwisho ,TOA MAONI yako hapo chini.

Sunday, April 26, 2020

FAIDA 15 ZA KUFUNGA KULA ZA KIAFYA

Watu wengi wanafahamu kuwa kufunga kula ni swala linalohusiana na imani zaidi. Wengi hawafahamu kuwa kufunga kula kuna manufaa ya kiafya pia.
🍏🍏Kufunga kula ni tendo lenye historia ndefu sana ambayo kimsingi chimbuko lake ni sababu za kiimani. Hata hivyo shuhuda na tafiti mbalimbali zimedhihirisha kuwa kuna manufaa mengine kemkem ya kufunga kula mbali na yale ya kiimani.
📒📒Ikiwa basi unapenda kuongeza maarifa pamoja na kuboresha afya yako, fahamu faida 15 za kufunga kula.

1. Huboresha metaboli

Metaboli ni mchakato ambao mwili hutumia virutubisho kutoka kwenye vyakula ili kujipa nguvu.
📒📒Unapofunga kwanza unapumzisha mfumo wako wa umeng’enyaji, pili unaufanya mchakato wa metaboli kwenda vizuri kwani mwili utatumia vyema virutubisho vilivyoko mwilini tayari.

2. Huboresha mzunguko wa damu

Tafiti mbalimbali zinaeleza kuwa kufunga kula hufanya mzunguko wa damu uende vizuri hasa kwa watu wenye aina ya pili ya ugonjwa wa kisukari (Type 2 Diabetes)

3. Husaidia kupunguza uzito

Kufunga kula ni njia mojawapo bora ya kupunguza uzito kwani kwa njia hii mwili hutumia mafuta yaliyoko mwilini ili kujipa nguvu.

4. Hufanya insulini kufanya kazi vizuri

Unapofunga kula mwili huzalisha insulini ili kutawala kiwango cha sukari mwilini kwani hakuna sukari inayoingia. Kwa njia hii insulini itaweza kuzalishwa na kufanya kazi ipasavyo mwilini mwako.

5. Hupunguza shinikizo la damu

Watu wengi wanapofunga hujikuta pia shinikizo la damu likipungua, hii inasababishwa na kupungua kwa kiwango cha chumvi kwenye damu.
Kumbuka chumvi nyingi husababisha shinikizo la damu. Hivyo kufunga ni kupunguza kiasi cha chumvi kinachoingia mwilini.

6. Husaidia kutawala sukari mwilini

Kwa watu wenye kiwango kikubwa cha sukari mwilini, wanaweza kutumia njia ya kufunga ili kukipunguza. Kumbuka unapofunga unapunguza pia kiwango cha sukari kinachoingia mwilini.

7. Hurefusha maisha

Watafiti wa afya wanaeleza kuwa kula sana kunakufanya pia uzeeke mapema. Wanaeleza kuwa kula kidogo kutatawala mchakato wa metaboli, hivyo kuzuia seli kuchakaa mapema.

8. Hukuwezesha kuhisi njaa

Kuna watu huwa wanashindwa kula vizuri kwa sababu huwa hawahisi njaa vyema. Njia moja wapo ya kupata njaa ambayo itakusababisha ule vyema, ni kufunga kula.

9. Huboresha utendaji kazi wa ubongo

Kufunga kula kunachochea uzalishaji wa protini ya brain-derived neurotrophic factor (BDNF) ambayo ni muhimu sana katika ukuaji, afya na utendaji kazi wa seli za fahamu za ubongo (neurons).

10. Huboresha kinga mwili

Kufunga kula hufanya kinga mwili kujiimarisha ili kukabiliana na chochote kinachoweza kutokea.
Hii ni kwa sababu unapofunga unabadili hali ya msingi ya mwili na inabidi kinga mwili kujiimarisha kujianda na lolote linalohusiana na mabadiliko hayo.

11. Huboresha afya na mwonekano wa ngozi

Ingawa lishe bora ni muhimu kwa ajili ya afya ya ngozi, kufunga kula kunaifanya ngozi iwe na mwonekano mzuri.
Ngozi inapokuwa na sukari nyingi, huifanya iwe na mwonekano usiovutia.
Kwa kufunga kula utapunguza kiwango cha sukari kinachoingia mwilini, hivyo kuwa na ngozi yenye mwonekano mzuri.

12. Huwezesha kujizalisha upya kwa seli

Seli hukua na kuchakaa au hata kufa kwenye mwili wa binadamu.  Kama ilivyo kwa kinga mwili, utafiti unaonyesha kuwa unapofunga mwili huzalisha seli mpya ili kujiaanda au kukabili badiliko lolote linaloweza kutokea.

13. Huboresha afya ya moyo

Watafiti wa afya wanaeleza kuwa kufunga kula kunasababisha mishipa ya moyo na misuli kufanya kazi vyema.

14. Husaidia Kutawala umbo la mwili na mwonekano

Njia nzuri ya kutawala umbo au mwonekano wako ni kwa kutawala kile unachokula. Hii ndiyo sababu walimbwende au warembo hujizuia sana kula hovyo ili wasije wakaharibu mwonekano wao.
Kwa njia ya kufunga kula utaweza kutawala umbo na mwonekano wa mwili wako kama unataka uwe mnene au mwembamba.
#Ya Ziada

15. Huokoa pesa

Hii ni faida ambayo siyo ya kiafya lakini inatokana na kufunga. Kama umezoea kununua chakula, mara ufungapo utaokoa pesa nyingi ambazo ungezitumia kwa ajili ya kula.
Naamini hii ndiyo sababu hata watu wenye bajeti ngumu hupunguza milo ya chakula ili waokoe pesa.
Kumbuka

Friday, April 24, 2020

JE WAJUA KWANINI CORONA SIO MWISHO WA DUNIA

🌍🌍🌏    CORONA_SIO_MWISHO WA_DUNIA
🌐🌐DUNIA   imepitia majanga magumu  mbalimbali ZAIDI ya hivi virus vya Corona  na Watu walikufa ZAIDI ya COVID-19 inavyo leta vifo Sasa ⚰️⚰️⚰️⚰️⚰️
👉👉Hutakiwi kuogopa Corona ila unatakiwa kujua njia sahihi za KUJIKINGA na Corona virus,ukiwa na hofu inafanya kinga za  mwili kupunguza ufanisi wake wa kazi.

🌍🌍COVID-19 ni nini?💊💊

Hiki ni kirusi kutoka katika familia kubwa ya virusi vya corona. Virusi vya corona vipo vya aina nyingi na vinaweza kusababisha mafua ya kawaida na pia mafua hatari kama Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS) NA Middle East Respiratory Syndrome (MERS). COVID19 ni vinasaba vipya ambavyo havijawahi kutokea hapo awali.

🦇Chanzo cha virusi vya corona inaripotiwa kuwa wanyama pori.🦇

🌍dalili ni pamoja na homa, kikohozi, kukosa pumzi na kupumua kwa shida.

🌏🌏Kwanini mlipuko huu sio mwisho wa dunia🌍🌍🔕🔕

Ugonjwa huu umeripotiwa kwanza December 31 mwaka jana, hii haimaniishi ulianza tarehe hio. Kuna uwezekano mkubwa watu walianza kusambaza virusi vya Corona mapema zaidi na kwa sababu wengi hupata dalili zisizo kali, zenye kufanana na mafua, wasijue wameambukizwa corona.

📜📄📒Kutoka katika ripoti ya chuo kikuu cha John’s Hopkin’s marekani takribani 3.7 % ya waliougua corona wamefariki. Maana yake ni kwamba takribani 96% ya wagonjwa watapona kabsaaaaaaa ✍️

✍️✍️Ukilinganisha na aina nyingine ya virusi vya corona kama SARS kiasi cha wagonjwa wanaofariki ni 10% (jumla ya wagonjwa waliofariki duniani ni 774) na MERS ni 34% (toka 2012 watu waliofariki wamefikia 858). Mafua ya msimu (seasonal flu) huko marekani yanauwa 0.1% ya wagonjwa.

🌏Kihistoria kuna magonjwa hatari zaidi yaliowahi kutokea📜📜

🌍Mwaka 1347 dunia ilikumbwa na ugonjwa wa tauni (The Black Death) ambayo inakadiriwa kuuwa watu kuanzia milioni 25 hadi milioni 200 sawa sawa na idadi  ya wa wananchi wote wa Nigeria leo hii.

🌍Mwaka 1918 janga la kidunia (pandemic) la mafua ya hispania (spanish flu) lilitangazwa. Mafua ya hispania yaliathiri watu milioni 500 na kuuwa takribani watu milioni 50 sawa na idadi ya watanzania.

🌍Mwaka 1968 mafua ya Hong Kong yaliuwa takribani watu milioni 1 hadi 4. Na janga la mwisho la kidunia kutangazwa na WHO kabla ya corona ni mafua ya nguruwe mwaka 2009 yalioathiri watu milioni 60 na kuuwa watu 12,469.

🌍🌍Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba dunia imepitia majanga mengi yaliokuwa na athari kubwa kwa uhai wa mwanadamu zaidi ya corona na tukashinda na Mwisho wa dunia haukutokea.
👩‍⚕️👩‍⚕️. Cha msingi ni kuendelea kusikiliza maelekezo kutoka katika mamlaka za afya, kufuata maelekezo ya kunawa mikono kwa sabuni au hand sanitizers, Kuvaa barakoa , kutosalimiana kwa kupeana mikono na kuripoti mgonjwa mwenye dalili tajwa.
🍎Pia kumuomba Mungu atupitishe kwenye janga hili Kama tulivyotoka hayo MENGINE 👩‍⚕️👩‍⚕️👩‍⚕️
🌍🌍Punguzeni hofu 🌏 my

Thursday, April 16, 2020

JE SIZE GANI YA UUME NI SAWA? (AVERAGE PENIS SIZE)

✍️Dr.chilo.MwanaApp 👩‍⚕️ online CLINIC
👩‍⚕️👩‍⚕️Ni swali ambalo wanume wengi wamekua wanajiuliza.je size ipi ya uume ndo tunasema ni sawa(normal or average), je ni size gani ya uume ndo inakua kibamia?

📚📚Kulingana na utafiti uliochapishwa kwenye harida la Madaktari wa mfumo wa uzazi wa wanaume La Uingereza (BRITISH JOURNAL OF UROLOGY INTERNATIONAL) soma nakala ya  utafiti HAPA
urefu wa  kawaida wa uume uliolala(flaccid penis) ni kuanzia inch 3.61 kuendelea na urefu wa uume uliosimama  ni kuanzia inch 5.16. Na unene wa kawaida wa uume uliolala ni kuanzia inch 3.66 wakati unene wa kawaida kwa uume uliosimama ni kuanzia inch 4.59.

📌📌Endelea kufatana nami ili kufahamu zaidi kuhusu size ipi ni sawa kwa uume,size ipi nzuri kwa kuridhishana wakati wa tendo la ndoa na kipi unaweza kufanya kama una wasiwasi na maumbile yako kuwa madogo.

📚📚TAFITI ZINASEMAJE🗣️🗣️

 Utafiti wa JARIDA LA MADAKTARI WA MFUMO WA UZAZI WA WANAUME ulitumia Majaribio takribani 17 na kuhusisha wanaume zaidi ya 15,000. Katika utafiti huu ilionekana kwamba 95% ya wanaume walikua na urefu wa inch6.3  na kwamba kati ya wanume 100 wanaume 5 tu ndo wana size zaidi ya inch 6.3. na asilimia 5% walionekana kuwa na uume wa inch 3.94,ikimaanisha kuwa wanaume 5 kati ya 100 wana uume chini ya inch 3.94.





JINSI YA KUPIMA SIZE YA UUME

💞💞Vipimo vya uume vipo vya aina mbili.wakati uume umelala na wakati uume umesimama.
Kuna urefu wa uume wakati umelala na urefu wakati uume umesimama,hivyo hivyo pia unene wakati uume umelala na unene wakati umesimama.

🌹🌹Kupima urefu wakati uume umelala na wakati umesimama chukua rula  unapima kuanzia kwenye mfupa wa Pubis(pubic bone) hadi ncha  ya kichwa cha uume.

Kupima unene chukua tape measure na pima mzunguko wa uume.



JINSI YA KUPIMA UREFU





JINSI YA KUPIMA UNENE







👌JE UNAWEZA KUONGEZA SIZE YA UUME?👌👌

Jibu ni ndio inawezekana,vipo vifaa maalum Vinajulikana kama penis vacum pumps na madawa mbali mbali ya kuongeza size ya uume lakini vitu hvi vina madhhara pia kwa mtumiaji.Yapo mazoezi maalumu ya kuongeza size ya uume ambayo nitaelezea katika makala inayofata.


😋😋Unapochagua njia ya kuongeza uume inapaswa kuwa makini na kuelewa kwa undani njia hiyo inafanyaje kazi na ina madhara gani.njia ya maozezi imeonekana kutokuwa na madhara.

USIYO YAJUA KUHUSU CORONA ,(COVID 19)

Usiyoyajua kuhusu Corona leo leo nimekuandalia makala hii ili ungundue mengi
✍️✍️1. Kwanza neno Corona.
Corona ni neno la Kilatini. Tafsiri yake kwa Kiswahili ni taji. Corona hutumika zaidi kuelezea “taji la mwanga” linalovika au linalotokana na nyota, jua au mwezi. Jua linapozama, unaona jua na duara la mwanga linalozunguka jua. Hilo duara ndio Corona.

2. Kwanini kuna virusi vimepewa jina hili? Kwasababu kuna familia kubwa ya virusi ambavyo ukivitizama kwenye microscope umbile lake linafanana na Corona. Virusi vya aina hii huruka kutoka kwenye wanyama (hasa popo) na kwenda kwenye binadamu), na sio lazima kwa kula wanyama hawa.

3. Katika familia kubwa ya mamia ya virusi vya Corona, aina saba ndio “zimeruka” kutoka kwa wanyama kwenda kwa binadamu. Kwahiyo, tukitafuta ufasaha, hakuna ugonjwa unaoitwa “Ugonjwa wa Corona”. Yapo magonjwa saba yanayosababishwa na aina moja au nyingine ya virusi vya Corona.

4. Katika aina hizo saba, maarufu ni virusi vitatu: cha kwanza kilipewa jina la MERS-CoV (Middle-East Respiratory Syndrome coronavirus) kilichoibukia Saudi Arabia mwaka 2012 na kuenea nchi 27 na kusababisha ugonjwa wa mfumo wa kupumua (MERS) uliowapata watu 2600 na kuuwa watu 866.

5. Kirusi cha pili cha Corona kilipewa jina la SARS-CoV-1 (Severe Acute Respiratory Syndrome coronavirus 1), kilicholipuka mwaka 2002 huko China na kuenea nchi 21 na kusababisha ugonjwa wa SARS unaoshambulia mfumo wa kupumua uliowapata watu 8,400 na kuua watu 813.

6. Kirusi cha tatu maarufu cha Corona ni hiki tulichonacho sasa. Jina lake rasmi ni SARS-CoV-2. Kimeibukia China mwaka 2019 na kuenea nchi 180 hadi sasa na kusababisha ugonjwa wa mfumo wa kupumua uliopewa jina la COVID-19 uliowapata watu 1,309,439 na kuwaua watu 72,638 hadi sasa.

7. Virusi vya SARS-CoV-1 na MERS-CoV vimedhibitiwa kwa sehemu kubwa ingawa bado hakuna tiba wala chanjo (kwa kudhibiti ueneaji wake) ingawa kwa asili havikuwa virusi vinavyoenea kwa haraka na kwa kasi. Virusi vya MERS-CoV vilikuwa hatari zaidi kwani 35% ya waliogua walifariki.

8. Kirusi hiki tulichonacho sasa kinaenea kwa kasi zaidi kwasababu: wanaoambukizwa hawaonyeshi dalili kwa muda mrefu na wanavisambaza kwa wengi huku wakiwa wazima. Pia kirusi hiki kinadumu (hadi siku kadhaa) kwenye vitu mbalimbali tunavyovigusa mara kwa mara (meza, n.k).

9. Kuhusu virusi kwa ujumla: Dunia hii ni ya virusi. Uzito wa virusi vyote duniani unazidi uzito wa binadamu. Hata hivyo asilimia kubwa ya virusi havina madhara. Hatari kubwa ya virusi ni kwamba bado hatujagundua vyote, na hatujui lini vipya vitalipuka na ukubwa wa madhara yake.




10. Kihistoria, binadamu amekabiliwa na majanga ya virusi mbalimbali yaliyoua mamilioni lakini amevikabili kwa chanjo, tiba na ujenzi wa kinga. Mfano virusi vya Rubeola vinavyoleta surua, virusi vya Variola vinavyoleta ndui, nk. Kwahiyo matumaini ya tiba na chanjo ya COVID19 yapo.

11. Lakini pia vipo virusi, kama vile HIV, vinavyosababisha UKIMWI, ambavyo tangu tuvijue miaka 35 iliyopita, pamoja na mabilioni ya dola kutafuta chanjo na tiba, hadi sasa hatujafanikiwa. Chanjo na tiba ya COVID19 inatafutwa kwa kasi, lakini hakuna uhakika wa mafanikio ya haraka.

12. Virusi pia huwa vina tabia mahsusi ya kujibadilisha, yaani mutation, na hivyo kujenga sifa mpya za kimaumbile/kibaiolojia. Jambo hili hufanya kazi ya kuudhibiti maambukizi au kutafuta tiba au chanjo kuwa ngumu. Kasi ya kujibadilisha inatofautiana kati ya aina ya virusi.

13. Dalili zinaonyesha kwamba kirusi hiki kinabadilika lakini sio kwa kasi kubwa. Mwisho, mambo mengi bado hayajajulikana kuhusu SARS-CoV-2 na COVID19, ikiwemo urahisi na uharaka wa aliyeambukizwa kuambukizwa tena akipona. Dawa kwa sasa ni kufuata maelekezo ya wataalam.

14. Zaidi: virusi ni vidudu vijanja sana. Vina-evolve na kujibadilisha ili viweze kusambaa kwa urahisi zaidi, kuleta madhara makubwa zaidi, na kuhakikisha haviuawi. Kuna virusi vikiingia vinashambulia au kupumbaza kwanza mfumo wa kinga. Ndio maana mapambano na virusi ni makali.

15. SARS-CoV-2 vikikuingia vinatulia kwenye koo kwanza ili ukikohoa vitoke na kufuata wengine. Ndo maana dalili ya kwanza ni kukohoa. Then vinajigandisha kwenye seli za mapafu na kujizalisha kwa mabilioni na kufanya mfumo wako wa kinga u-overheat kiasi kwamba hiyo tu inakuuguza.

Saturday, April 11, 2020

Athari Za Kufanya Mapenzi Kila Siku

✍️Kuna watu ambao hawawezi kulala bila kufanya mapenzi na huku wengine wakikosa uwezo wa kuvumilia hata kwa siku mbili au tatu.
🌺kawaida kufanya mapenzi kuna faida Nyingi, lakini linapo kuja swala la kuzidi kiasi tunapata matatizo ya msingi ambayo huleta madhara kwa watu wanaoendekeza sana ngono.

Mtu anaweza kuwa na mke na kujikuta kilia siku ‘anahondomola’ kwa sababu tu hakuna wakumkataza na kwamba anahaki ya kufanya hivyo kwa sababu amelipa mahari.

Imeelezwa kuwa watu wengi kati ya watu wanao lalamika kupoteza hisia za kimapenzi hutoka katika kundi la watu wapenda ngono.

Si kila unapokutana na mwenza wako basi mshiriki tendo la ndoa kwani kwani kufanya hivyo ni sawa na kujikomoa mwenywe. Miongoni mwa madhara ni pamoja na;-


Kupoteza hamu ya tendo

💝💝Watu wenye pupa za kufanya mapenzi hupoteza haraka hisia za kufanya mapenzi kwa wenzi wao kutokana na sababu za kisaikolojia zinaweza kujitokeza wakati wa kufanyaji wa tendo la ndoa mara kwa mara.

Sababu hizo ni pamoja na zile za kumzoea mwenza kiasi chakukosa msisimko hata Anapo muona akiwa mtupu.

Aidha kukinai haraka staili za kimapenzi kunatajwa kujitokeza. Kutokana na kukutana mara kwa mara kwa aina zile zile za mapenzi napengine kitanda kimoja au chumba kile kile ,jambo ambalo linaweza kumfanya muhusika asione jipya kutoka kwa mwenza wake na hivyo hupoteza hamu naye na kihisi kama hawezi kushiriki tendo la ndoa kikamilifu.

Kuujaza mwili tamaa kubwa
💝💝Tabia ya kufanya mapenzi mara kwa mara huongeza uzalishaji wa homoni mwilini uwe na msukumo mkubwa wa kutaka kuridhishwa kwa tendo la ndoa bila kukosa na hivyo humfanya mhusika asiwe mtu mwenye uwezo wa kuzuia tamaa na kukosa chaguo la nani wa kufanya nae mapenzi na kwa wakati gani.

Watu wanaojiendekeza katika kufanya mapenzi mara kwa mara ndio wale ambao kila wanae mtazama barabarani humtamani bila kujali hadhi yake au afya yake.

Unakuwa mtu wa kufanya mapenzi mara kwa mara huwezi kuwa na uwezo wakuizuia tamaa yako mwenza wako akiondoka siku mbili utatamani uwe na yeyote aliye karibu yako ili akukate kiu ya penzi.



Kupoteza raha kamili ya tendo

💞💞Raha ya tendo hutegemea na hisia iliyo kuzwa kutokana na mapenzi sahihi au kuwa na kiu ya kufanya mapenzi,hivyo basi ukiwa mtu wa kufanya mapenzi kila mara unaweza kupoteza msisimko wa tendo na kujikuta unapata furaha ambayo haikutoshi kumaliza tamaa yako.

Kama ni mapenzi utakua unafanya kwa mazoea tu na msisimko wako utakuwa mdogo.

Kupoteza nguvu za mwili


💞Maengine yanayo weza kupatikana kwa kufanya mapenzi mara kwa mara ni pamoja na kupoteza nguvu nyingi za mwili.

Kama tujuavyo tendo la ndoa hasa kwa wanaume huwafanya watumie nguvu nyingi,hivyo huufanya mwili uchoke.

Aidha lishe inapo kuwa ndogo kwa wafanya mapenzi mwili hukosa nguvu za kutosha kuhimili misukosuko ya kimaisha.

Sambamba na hivyo mbegu za uzazi zinazotoka kwa wanaume wafanyao mapenzi mara kwa mara huwa dhaifu.

Kupata magonjwa

💞💞Wanaofanya mapenzi mara kwa mara huwa holela ambayo huweza kuwa sabababishia magonjwa ya zinaa ukiwemo ukimwi,lakini ufanyaji wa mapenzi usiyo kuwa na msukumo wa kutosha hasa kwa wana wake huwa fanya waishiwe misisimko na huzifanya sehemu zao za siri kutotoa ute unao weza kuwakinga na michubuko wakati wakujamiiana na hivyo huwa sababishia michubuko itayoweza kuleta maambukizi ya haraka ya magonjwa ya zinaa na ukimwi ukiwemo.

Friday, April 3, 2020

🥒 JUA  MAPEMA MADHARA YA KUNYONYA UUME/UKE!!!🍎


✍️MwanaApp ♥️ online clinic⚕️

🍎🍎 Kitendo hiki ni pale mwanamke anapoweka uume wa mwenza wake mdomoni mwake na kuanza kunyonya kama pipi  /mjini wanaika kulamba coni au mwanaume kuingiza ulimi ukeni pamoja na kunyonya via vya mwanamke (😋kuzama chumvini) pindi wapenzi hawa wawapo faragha.

👌👌Kumekua na ongezeko la kitendo hiki kwa vijana na imekua kama ni sehemu ya mahaba kwa wapenzi hata inafikia hatua mwanaume ANAONA MKE/MPENZI WAKE Ni (Mshambaa) HAJUI MAHABA KAMA HAJAMNYONYA UUME AU MWANAMKE KUONA HIVYO ASIPONYONYWA YEYE.VILE VILE KUNA WANAWAKE WANAONA KUFANYA MAPENZI BILA KUNYONYA NI USHAMBA.😎"Et MAPENZI UCHAFU".

😍Vyumbani mambo mengi sana hutokea katika suala zima la mapenzi, nitaenda kusema kwa ufupi madhara ya kunyonya.

1.KISONONO CHA KOO.
Kama unafanya hiki kitendo halafu ukute mwanamke/mwanaume ana magonjwa ya zinaa kama kisonono inakua rahisi kwa mnyonyaji kuambukizwa. Kumbukeni kama mwanamke ana kisonono sio rahisi kumgundua kama ilivyo kwa mwanaume.

 2.SARATANI YA KOO.
Hii hasa huwapata wanawake ambao hupenda kunyonya uume wanaume wengi na hivyo kuwaweka katika hatari ya kuambukiwa vimelea wanaosababisha saratani hiyo mfano HPV.

3.KUBADILISHANA VIJIDUDU (BACTERIA ).
Kama wote tunavofahamu ya kwamba kwenye miili yetu kuna vijidudu (bacteria) Rafiki (normal flora); sasa hao bacteria wakiingia sehemu ambayo sio yake huleta madhara kwani wameingia eneo ambalo hawajazoea, wataingia sehemu mpya kwa kuwanyonya kutoka kwa mwanamke au mwanaume. Hii inaweza isilete madhara mapema lakini uendeleaji wa kunyonya nyonya wanaume au wanawake wengi mara kwa mara hupelekea kupata madhara mengi na mengine ni magumu kutibu.

4. Kupata madonda mdomoni.

5. Kujiweka katika hatari ya kupata saratani za mdomo, ulimi  na Koo pale unapokuwa unameza maji maji ya sehemu unayoinyonya.nk.

🤔🤔Kupitia hili pia ijulikane kwamba mwili una bacteria wa faida ambao kitaalamu hutambulika kama Normal flora.

🍎🍎Normal flora hao wapo mdomoni, Ukeni (Wa ukeni husafisha uke na kuweka mazingira ya ukeni tofauti na sehemu zingine ), Puani, Na maeneo mengine.

🍓🍓Normal flora wa Mdomoni akienda Ukeni husababisha matatizo ya kiafya halikadhalika kwa normal flora wa Ukeni wakienda mdomoni husababisha maradhi.

🍏🍏Mbadilishano huo hupekekea kuzaliwa kwa maradhi sugu yasiyopona.

Utashangaa siku hizi watu wa natumia dawa za kupambana na harufu mbaya ukeni/kutokwa na uchafu ukeni wanapata nafuu na hali inajirudia bila kupata ata ahueni wasijue huenda wanatibu huku wanaambukiza tena,  Inakua ngumu kupona!!!!!

🌺🌺Kama unatatizo la uchafu ukeni na harufu mbaya ukeni fika hospitali upimwe tatizo hilo linatokana na nini, utapewa dawa tumia dozi ipasavyo kama unatabia hiyo ya kunyonyana acha uone kama tatizo litajirudia au laa.

🍎KWELI WANASEMA MAPENZI UCHAFU ILA USALAMA WA AFYA NI MUHIMU.👌
🗣️🗣️Toa maoni yako hapo chini