Monday, April 27, 2020

🤫Maneno 20 Ambayo Hutakiwi Kumwambia Mtoto Wako🤐


🎯Mara kadhaa wazazi wamekuwa wakiwaambia watoto wao maneno mbalimbali wakati wakiwa na furaha au hasira. Ipo nguvu kubwa kwenye maneno ya kutamkiwa ambayo wazazi wengi hawaifahamu.

💡 Kuna Siri kubwa kwenye kauli unazozitoa juu ya maisha yake ya baadae , hakika maneno yanaweza kujenga au kubomoa maisha ya mtoto kwa kiasi kikubwa.
 🤐 fahamu maneno 20 ambayo hutakiwi kumwambia mtoto wako.🎯

🤐1. Wewe ni mtoto mbaya🤫

Wazazi wengi wanapokasirishwa na mtoto humwambia wewe ni mtoto mbaya, hili humfanya mtoto ajione hafai na itamjengea kutojiamini .

🤐2. Kwanini usiwe kama dada au kaka yako?🤔

🎯Kauli hii humfanya mtoto ajione dhaifu kwa sababu unamlinganisha na wengine. Kauli hii pia humjengea chuki na wivu kwa wale unaowataja kwake kuwa ni bora. Hili husababisha watoto kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na kutopeana ushirikiano Siku wakiwa Wakubwa. pia MTOTO ataona ndani ya familia Kuna ubaguzi.

🤫3. Huwezi hili /unajisumbua tuu🤐

🎯Mwache mtoto ajaribu ashindwe na si wewe kumwambia kuwa hawezi.
"kwani kwenye maisha ni bora ujaribu na ushindwe kuliko kushindwa kujaribu." 💪kama mzazi unapaswa kuwa hamasa kwa mtoto na si kumkatisha tamaa.

🤐🤐4. Usiongee na mimi Tena ukome.

 🤔🤫Kama hautaki mtoto wako aongee na wewe, je unataka aongee na nani? Ukiwa umekwazwa na mambo yako, usihamishie matatizo hayo kwa mtoto.hii itamfanya atengeneze usugu  wa dharau na kibuli kwako mwenyewe.
♥️♥️Kumbuka mtoto naye ana haki ya kusikilizwa, msikilize na umjibu kama inavyotakiwa.

🤐🤐5. KWANINI UNAFANYA VITU KAMA MWANAMKE   ??🤔

🎯👉Kumwambia mtoto neno hili ni kumwonyesha kuwa kuna jinsia fulani bora au yenye nguvu zaidi. Hivyo ni vyema kutokumwambia mtoto neno hili, mwache akue na atatambua mwenyewe kama kuna jinsia dhaifu au yenye nguvu zaidi.

🤐🤐6. Niache/ Usinisumbue🤫🤫

🎯Wazazi wengi hupenda kuwaambia watoto wao “niache” “nina kazi niache” “usinisumbue”, n.k. Kumbuka kuwa wewe ni kila kitu kwa mtoto wako, je unataka akuache aende kwa nani?

🌱🌱Tenga muda na uwe karibu na mtoto wako na kuweza kusikiliza hisia zake.hapo utaweza kugundua kipaji Cha mtoto wako.

🤐7. Hakuna mtu anamtaka mtoto kama wewe ,kwanza sikupendiii🤫

🎯🎯Kuna wazazi huwajengea watoto roho ya kukataliwa tangu wakiwa wadogo sana. Kumwambia mtoto maneno haya humfanya ajione duni na mwenye kukataliwa; hivyo epuka maneno haya ili umkuze mtoto wako VIZURI nae aje akukumbuke ukiwa mzee.

🎯🎯8. Umeshakuwa usifanye Kama MTOTO.👇👇

✍️✍️Kama mtoto anamalizia utoto wake mwache amalizie asije akacheza ukubwani. Mwache afurahie na kuutumia utoto wake vyema kwani kuna kipindi ataacha utoto yeye mwenyewe. usilazimishe kila Kitu akifanye kwa muda unaoutaka wewe.

💪💪9. Wewe ni mvivu/ Ujiwezi /huna unachokijua wewe.

🏋️🏋️Mtoto akishatambua kuwa wewe unamwona ni mvivu, kamwe hawezi kuwa na bidii ya kazi. Mtoto anaposhindwa kufanya kazi vyema, mhamasishe na kumtia moyo badala ya kumwambia wewe ni mvivu / upokama mlenda mlenda tuuu .

😫10. Unaninyima raha wewe mtoto hujui tuuu😏😏

Mara nyingi watoto wanapowakwaza wazazi, wazazi huwaambia kuwa wanawanyima raha. Je kama unamwambia mtoto kuwa yeye siyo chanzo cha furaha kwako ni nani atakayekupa furaha?
😠 itamjengea hofu kila atakapo Kuwa Karibu yako na hawezi kukupaushirikiano wa maono na fikra zake.🙆🙆

🐓11.  lazima ufuate sheria zangu 🤛

🎯 Wazazi Wengi hujifanya mabepali/ na kutangaza utemi kwa WATOTO wao sio zuri kabsa  mpe nafasi Mtoto Kuwa huru kifikra.
🎯utamfanya Mtoto asiwe na uamuzi juu ya maisha yake na Kuwa mtumwa wa fikra zako 👣👣


🎯🎯12. Mali zote hizi Ni zako na nitakufanyia chochote unachotaka.🤸

🧠Inawezekana una mali nyingi ambazo kweli kabisa ni za mtoto wako, lakini unapaswa kumjengea mtoto akili ya kutafuta na si kumpumbaza kwa mali ulizo nazo.🧠🎯

Kumwambia mtoto kila kitu changu ni chako, humfanya asifanye bidii au aone ana haki ya kupata na kutumia kila kitu jinsi apendavyo, utaweza ukaja kujuta baadae kwa Maneno yako .


💖💖13. Nakupenda kuliko watoto wangu wote 💯💯

💘💘 Waswahili wanasema unampa bichwaaaa na kujiona keki .
Kauli hii humfanya mtoto awe mbaguzi na aone kuwa kuna ubaguzi na upendeleo kwenye familia. Hata kama unampenda mtoto fulani zaidi, basi usimwambie mtoto mwingine.
😁😁kauli zako Kuna Siku zitakukosesha Amani🙄🙄

😜14. Siwezi kukukatalia kitu .

🍎🍎 Kauli hii ni mbaya humfanya mtoto akutawale na aone kuwa unatakiwa kutii, kukubali na kumpa kila anachokitaka.kama unaijua kesho yako Basi endelea kumwambia hilo neno🌓


🙋15. Usiongee  au  Usiwatembelee Watu fulani fulani .

HakunaKitu kibaya Kama kurithishwa MAADUI.
Kama una chuki zako, zimalize wewe mwenyewe na si kuzihamishia kwa mtoto. Mtoto anapokuja duniani hutafuta kujenga mahusiano na watu na si kujenga chuki na matengano.

🤲🤲16. Sitakusamehe milele🤝🤝

"Kusamehe mtu aliyekukosea Kuna msaada mkubwa kwa Afya yako ulie samehe kuliko aliyekukosea._"

🙏🙏Mzazi anapaswa kuwa mfano mzuri wa kumfundisha mtoto kusamehe. Ikiwa wewe humsamehi anapokukosea, je unafikiri atakuwa na roho ya kusamehe wengine? Mfundishe mtoto kusamehe.👌👌

🤜17. Ngoja Mtu fulani aje akupige .💔

💗Hii ni kauli inayopendwa sana na wazazi wengi hasa wakina mama ,mama usitengenezee chuki kwa watu wengine 👉 timiza wajibu wako🙋.
Kauli hii humfanya mtoto amwogope baba na amwone kama adui, pia humfanya mtoto amwone mama kuwa ni dhaifu, ikiwa baba hayupo mtoto atafanya makosa kwani anajua mama hamfanyi kitu chochote na hatuwezi.

😥18. Matusi yote  na Majina mabaya.

🎯Mtoto mtukanaji mara nyingi anaishi kwenye familia inayotukana. Utamkuta mama anamwita mtoto mbwa ,mbuzi, ng’ombe, shetani, jambazi, paka, nguruwe,  n.k. je kweli ulizaa vitu hivyo Basi Kama yeye mbwa, Basi wewe utakua mama mbwa Sasa. 🙄Jiulize tuu Siku  akujibu  hata wewe mbwa 👉 Kama unavyoniita👌👌.
Kama nakuona vile itakavyo kuchoma Basi tuache kuita WATOTO Majina mabaya.
📖📙Unapomtukana mtoto, naye hujifunza kuwatukana watu wengine na Siku atakutukana wewe pia mbele za watu. Pia humwathiri kisaikolojia na kiroho na kumfanya awe kama kile unachomwita.

🔪🔪19. Nitakumaliza au nitakuua🔪

Baadi ya wazazi huenda mbali zaidi na kuwaambia watoto wao maneno ya kuwatishia kuwadhuru vibaya au kuwaua.

Hili humwathiri mtoto kisaikolojia na kumjengea tabia ya kuwatishia au kuwadhuru watu wengine. Kama mtoto anatishiwa kuuwawa na wewe ni nani atakayemlinda?
 💡chunga ulimi wako👅


20. Acha kulia haraka au usilie

👁️Kulia ni njia moja wapo ya mtoto kueleza hisia zake. Kumzuia mtoto kulia ni sawa na kumkataza kuweka wazi hisia zake. Mwache alie kama hana maradhi, kwani baada ya muda atachoka na kunyamaza mwenyewe.
Kitendo Cha kulia hata kwa watu wazima HUONGEZA Siku za kuishi.
💡Muombe Mungu akujaria hekima,busara na maarifa ya kumkuza mtoto kwenye tabia unayoipenda *
🎯MUNGU ATIMIZE HITAJI LA MOYO WAKO🙏🙏
✍️✍️DR.CHILO.💡 Asante kwa kusoma hadi Mwisho ,TOA MAONI yako hapo chini.

No comments:

Post a Comment