🌍🌍🌏 CORONA_SIO_MWISHO WA_DUNIA
🌐🌐DUNIA imepitia majanga magumu mbalimbali ZAIDI ya hivi virus vya Corona na Watu walikufa ZAIDI ya COVID-19 inavyo leta vifo Sasa ⚰️⚰️⚰️⚰️⚰️
👉👉Hutakiwi kuogopa Corona ila unatakiwa kujua njia sahihi za KUJIKINGA na Corona virus,ukiwa na hofu inafanya kinga za mwili kupunguza ufanisi wake wa kazi.
🌍🌍COVID-19 ni nini?💊💊
Hiki ni kirusi kutoka katika familia kubwa ya virusi vya corona. Virusi vya corona vipo vya aina nyingi na vinaweza kusababisha mafua ya kawaida na pia mafua hatari kama Severe Acute Respiratory Syndrome (SARS) NA Middle East Respiratory Syndrome (MERS). COVID19 ni vinasaba vipya ambavyo havijawahi kutokea hapo awali.
🦇Chanzo cha virusi vya corona inaripotiwa kuwa wanyama pori.🦇
🌍dalili ni pamoja na homa, kikohozi, kukosa pumzi na kupumua kwa shida.
🌏🌏Kwanini mlipuko huu sio mwisho wa dunia🌍🌍🔕🔕
Ugonjwa huu umeripotiwa kwanza December 31 mwaka jana, hii haimaniishi ulianza tarehe hio. Kuna uwezekano mkubwa watu walianza kusambaza virusi vya Corona mapema zaidi na kwa sababu wengi hupata dalili zisizo kali, zenye kufanana na mafua, wasijue wameambukizwa corona.
📜📄📒Kutoka katika ripoti ya chuo kikuu cha John’s Hopkin’s marekani takribani 3.7 % ya waliougua corona wamefariki. Maana yake ni kwamba takribani 96% ya wagonjwa watapona kabsaaaaaaa ✍️
✍️✍️Ukilinganisha na aina nyingine ya virusi vya corona kama SARS kiasi cha wagonjwa wanaofariki ni 10% (jumla ya wagonjwa waliofariki duniani ni 774) na MERS ni 34% (toka 2012 watu waliofariki wamefikia 858). Mafua ya msimu (seasonal flu) huko marekani yanauwa 0.1% ya wagonjwa.
🌏Kihistoria kuna magonjwa hatari zaidi yaliowahi kutokea📜📜
🌍Mwaka 1347 dunia ilikumbwa na ugonjwa wa tauni (The Black Death) ambayo inakadiriwa kuuwa watu kuanzia milioni 25 hadi milioni 200 sawa sawa na idadi ya wa wananchi wote wa Nigeria leo hii.
🌍Mwaka 1918 janga la kidunia (pandemic) la mafua ya hispania (spanish flu) lilitangazwa. Mafua ya hispania yaliathiri watu milioni 500 na kuuwa takribani watu milioni 50 sawa na idadi ya watanzania.
🌍Mwaka 1968 mafua ya Hong Kong yaliuwa takribani watu milioni 1 hadi 4. Na janga la mwisho la kidunia kutangazwa na WHO kabla ya corona ni mafua ya nguruwe mwaka 2009 yalioathiri watu milioni 60 na kuuwa watu 12,469.
🌍🌍Ninachojaribu kusema hapa ni kwamba dunia imepitia majanga mengi yaliokuwa na athari kubwa kwa uhai wa mwanadamu zaidi ya corona na tukashinda na Mwisho wa dunia haukutokea.
👩⚕️👩⚕️. Cha msingi ni kuendelea kusikiliza maelekezo kutoka katika mamlaka za afya, kufuata maelekezo ya kunawa mikono kwa sabuni au hand sanitizers, Kuvaa barakoa , kutosalimiana kwa kupeana mikono na kuripoti mgonjwa mwenye dalili tajwa.
🍎Pia kumuomba Mungu atupitishe kwenye janga hili Kama tulivyotoka hayo MENGINE 👩⚕️👩⚕️👩⚕️
🌍🌍Punguzeni hofu 🌏 my
No comments:
Post a Comment